Karibu
SOHEECO Projects

Tunaboresha Maisha ya Mtu Binafsi, Jamii, Shule/ taasisi na Familia.

Kuhusu SOHEECO Projects

Karibu SOHEECO Projects kituo na jukwaa sahihi kwako lililosajiliwa kisheria (BRELA Na. 638459 na TIN: 145-067-693), ambapo mabadiliko hukutana na mafanikio! Unadhani ni UTANI? Endelea kusoma na kutufatilia!

Dhamira yetu ni kuhamasisha, kuelimisha, na kuwawezesha watu binafsi, jamii, shule, na taasisi nyingine katika nyanja za Kijamii, Afya, na Uchumi (SOHEECO). Sisi ni chanzo kinachoaminika cha mwongozo wa vitendo na suluhisho bunifu zilizobuniwa mahsusi ili kuimarisha mahusiano, kuboresha afya, na kufanikisha mafanikio ya kiuchumi.

KIJAMII: Mahusiano, Ndoa na Familia

Tunaamini kuwa mahusiano imara ndiyo msingi wa jamii zinazostawi. Maeneo yetu ya mkazo ni:

  • Ushauri wa Ndoa na Mahusiano: Kuimarisha uaminifu na mawasiliano.
  • Mienendo ya Familia: Kutatua migogoro na kujenga mazingira ya nyumbani yenye afya.
  • Ustawi wa Hisia: Kujenga ustahimilivu kupitia changamoto za maisha.

​​KIAFYA: Ustawi na Lishe

Afya njema ni nguzo ya ustawi wa maisha. Tunatoa huduma na elimu kuhusu:

  • Kinga dhidi ya Magonjwa: Kupunguza hatari za kiafya kwa mikakati ya vitendo.
  • Lishe Bora: Kufuata mlo kamili na tabia endelevu za ulaji.
  • Tiba Asilia: Kuzitumia kikamilifu mbinu za kiafya za asili.

KIUCHUMI: Uhasibu, Fedha, Kilimo, Uchumi wenyewe, Manunuzi, Mauzo, Usimamizi, na Biashara/ Ujasiriamali

​Mafanikio ya kiuchumi huanzia na mikakati sahihi na usimamizi bora. Tunashughulikia maeneo yafuatayo:

  • Uhasibu na Fedha: Uandaaji wa bajeti, uhasibu wa kila siku, na uzingatiaji wa sheria za kodi kwa watu binafsi na wafanyabiashara.
  • Kilimo: Kilimo endelevu, usimamizi wa mazao, na matumizi ya mbinu bunifu kwa wakulima.
  • Uchumi: Uelewa wa masoko, mwenendo wa kiuchumi, na athari za sera.
  • Manunuzi: Usimamizi wa rasilimali kwa ufanisi na mikakati ya mnyororo wa ugavi.
  • Mauzo: Mbinu za kuuza bidhaa na huduma kwa ufanisi, ujenzi wa mahusiano na wateja, matumizi ya masoko ya kidijitali (digital marketing), na kuongeza mapato ya biashara.
  • Usimamizi: Ujuzi wa uongozi, mikakati ya uendeshaji wa taasisi, na kufanya maamuzi yenye tija.
  • Ujasiriamali: Kuanza na kukuza biashara hata kwa rasilimali chache.

Katika SOHEECO Projects, tunachanganya utaalamu kutoka vitengo vitatu: 

  1. SOHEECO JAMII (FUHUWI – masuala ya kijamii yaani mahusiano, ndoa na familia),
  2. SOHEECO AFYA (FUHUWI – masuala ya kiafya yaani ustawi wa afya na lishe)
  3. SOHEECO UCHUMI (ACAMABECA – masuala ya kiuchumi yaani Uhasibu, Fedha, Kilimo, Uchumi wenyewe, Manunuzi, Mauzo, Usimamizi, na Biashara/ Ujasiriamali)

Pamoja, tunakuwezesha kufanikisha mabadiliko ya maana katika kila nyanja ya maisha.

Karibu tupige hatua kwa pamoja — hatua moja karibu zaidi na maelewano ya kijamii, afya bora, na uhuru wa kiuchumi.

Jiunge nasi katika kujenga maisha yenye afya, nguvu na mafanikio zaidi!

Historia ya SOHEECO PROJECTS

SOHEECO PROJECTS ilianza kama wazo, lakini lenye dhamira kubwa ya kubadilisha maisha ya watu kijamii, kiafya na kiuchumi. Historia yenyewe ni kama ifuatavyo;

21 Novemba, 2017 – Kuzaliwa kwa Vision to Money (VITOMO), likiwa na lengo la kuwahamasisha vijana kubadilisha mawazo kuwa maono, na maono kuwa matokeo (pesa). Pamoja na uwepo wa Facebook Page, utekelezaji ulikuwa mdogo kutokana na changamoto za vitendea kazi.

8 Januari, 2019 – VITOMO ikabadilika kuwa FUHUWI (Future Husbands and Wives), ikilenga kusaidia vijana kushinda changamoto za mahusiano, kupata wenza sahihi, na kujenga ndoa na familia bora kupitia WhatsApp Groups na Facebook Pages kwa njia ya mafunzo, ushauri na mijadala ya pamoja.

8 Aprili, 2021 – FUHUWI ikapanuliwa kuwa Future Husbands and Wives Consultation Centre, kuongeza weledi na upana wa huduma za ushauri, huku ikiendelea kutumia majukwaa ya mtandaoni kuwafikia watu wengi zaidi.

5 Machi, 2022 – Kuanzishwa kwa ACAMABECA (Accountant and Manager, The Beloved Careers) kupitia Facebook Pages, ikiwa na lengo la kusaidia vijana, familia na taasisi kusimamia fedha vizuri (matumizi ya fedha makubwa kuliko kipato), kupunguza madeni, na kuongeza mali pamoja na vyanzo vya kipato (ili kupunguza madeni huku matumizi yakidhibitiwa).

23 Februari, 2023 – ACAMABECA ikaboreshwa kuwa Accountant And Manager, The Beloved Careers Enterprise, ikiimarisha utoaji wa huduma za ushauri na makala zenye mafunzo mahususi kwa maendeleo ya kifedha.

6 Agosti, 2024 – FUHUWI ikaongeza huduma za afya (lishe na virutubisho), kwa kutambua mchango mkubwa wa afya katika ustawi wa mahusiano, ndoa na familia kwani changamoto za afya (lishe) zinaweza kuchochea changamoto za mahusiano, ndoa na familia.

25 Desemba, 2024 – Kuundwa kwa SOHEECO PROJECTS (Social, Health & Economic Projects) kwa kuunganisha huduma zote za Jamii na Afya (FUHUWI) pamoja na Uchumi (ACAMABECA) chini ya mfumo mmoja.

20 Januari, 2025 – Kuzinduliwa kwa tovuti ya SOHEECO PROJECTS (soheecoprojects.com) kwa ajili ya kuwasilisha huduma kwa mpangilio bora zaidi, ikijumuisha makala za kila wiki, ushauri wa kitaalamu, mifumo (Apps & Tovuti) na bidhaa mbalimbali yaani e-Books, mbolea ya SuperGro na Virutubisho Lishe. Walengwa wakiwa ni kwa waajiriwa, waajiri/ wamiliki, wafanyabiashara, wakulima, wanandoa, vijana walioko kwenye mahusiano, na wagonjwa wa magonjwa sugu (yasiyoambukiza).

Leo, SOHEECO PROJECTS inaendesha huduma zake kupitia vitengo vitatu:

SOHEECO JAMII (FUHUWI), SOHEECO AFYA (FUHUWI), na SOHEECO UCHUMI (ACAMABECA)

– vyote vikifanya kazi kwa pamoja kutoa suluhisho jumuishi ndani ya jukwaa (tovuti) moja.

Kwa kipindi chote hiki, WAZO limeendelea kukua kutokana na mahitaji halisi ya jamii kuwa KITUO na JUKWAA na kusababisha uwekezaji unaoendelea katika huduma na bidhaa zenye lengo la kutoa matokeo halisi kwa wateja na wadau wa SOHEECO kwa ujumla.

Maeneo Muhimu Katika Tovuti Yetu

1. Ni wapi pa Kupata Zana za Kujifunzia Kidigitali kwa Shule Nchini Tanzania ?

Kupitia SOHEECO Projects, unaweza kupata aina mbalimbali za vitabu pepe (eBooks), makala za elimu na maarifa, na zana za kujifunzia mtandaoni na nje ya mtandao vinavyofaa kwa shule, walimu, na wanafunzi nchini Tanzania.

📚 Maktaba Yetu (PDF, ZIP na Zana Mbalimbali): Bofya hapa

🛒 Duka letu: Bofya hapa

📝 Blogu Yetu (Makala za Elimu na Maarifa); Bofya hapa

Zana hizi zinaweza kusaidia ufundishaji darasani, kujisomea nyumbani, na maktaba za shule—vikijumuisha masomo yanayolingana na mahitaji ya elimu nchini Tanzania.

2. Ni wapi unaweza kununua virutubisho vya asili na kupata mafunzo mtandaoni nchini Tanzania?

Kupitia SOHEECO Projects, unaweza kununua “Supplements Asilia” na  mafunzo mtandaoni;

CEO & Founder
Francisco J. Kagoma

Mwasisi (Founder) na Mkurugenzi (CEO) | SOHEECO PROJECTS

Ni mtaalamu wa uhasibu na usimamizi mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 7 katika shule binafsi. Kupitia SOHEECO PROJECTS yaani FUHUWI CONSULTATION CENTRE na ACAMABECA ENTERPRISE, amejikita katika kutoa maarifa ya kiutawala, kifedha, kiuchumi, na maendeleo ya taasisi kwa njia ya elimu, ushauri na maandiko ya kitaalamu. Pia anatoa maarifa na ushauri kuhusu lishe bora, magonjwa yasiyoambuzika, mahusiano, ndoa na familia. Pia ni Mjenzi na Mbunifu wa Tovuti (Website Developer & Designer) ya SOHEECO Projects. Tovuti ya SOHEECO Projects ni moja ya kazi zake (https://soheecoprojects.com)

Ni mume wa mke mmoja (1) na watoto wawili (2).

Deputy CEO

Sylvia Temu

Mkurugenzi Msaidizi (Deputy CEO) | SOHEECO PROJECTS

Ni mzoefu mkubwa katika masuala ya ujasiriamali, ya kujitolea kwa huduma za kijamii, na kwenye maono ya pamoja kuhusu uwezeshaji kupitia mifumo ya kidijitali. Uzoefu wake unakamilisha uwezo wa Mkurugenzi katika masuala ya kifedha na mikakati, hivyo kutuwezesha kujenga timu ya uongozi iliyo imara, yenye uwiano na ufanisi katika kuendeleza SOHEECO PROJECTS. Uzoefu wake katika mahusiano unakamilisha Timu ya SOHEECO Projects na kuifanya itimize dhamira yake.

Ni mke wa mume mmoja (1) na mama wa mtoto mmoja (1).

Karibu SOHEECO Projects

Mahali pa kupata Afya Bora, Maarifa Sahihi na Mbinu za Kujitegemea.

Chagua unachotaka kuanza nacho:

Hapana, Nitasoma Makala Kwanza

Karibu tena SOHEECO 👋

Tuliona ulitembelea tovuti yetu lakini hujachagua bado.

Hapana, Labda Baadaye
SOHEECO PROJECTS

SOHEECO PROJECTS

Kwa kawaida majibu hutolewa ndani ya saa moja.

I will be back soon

SOHEECO PROJECTS
“Habari 👋
Ni rafiki yako Francisco J. Kagoma, CEO & Founder | SOHEECO PROJECTS. Naweza kukusaidia vipi?”
WhatsApp